Ni nini kinachohitajika ili kugundua IBD?

Ikiwa daktari wako anashuku kuwa una Ugonjwa wa Uvimbwe wa Matumbo au Ugonjwa wa Crohn unaweza kulazimika kufanyiwa vipimo na uchunguzi ili kuthibitisha utambuzi. Hakuna kipimo cha kipekee kinachoweza kutumika ili kufanya uchunguzi wa IBD. Daktari atatumia mchanganyiko wa vipimo ili kuthibitisha utambuzi.

VIPIMO VYA DAMU NA KINYESI

Vipimo vya damu vinaweza kuonyesha kama una uvimbe (CRP au ESR ya juu) mahali fulani katika mwili wako na kama una upungufu wa damu (himoglobini ya chini), zote mbili zinazopatikana kwa wagonjwa wenye IBD. Vipimo hivi pia vinaweza kutambua kama viungo kama vile ini na figo vinafanya kazi ipasavyo na kama kuna upungufu wa madini au vitamini.

Vipimo vya kinyesi vinaweza kutumika kutambua dalili za upungufu wa damu au uvimbe (calprotectin), na kuangalia kama kuendesha kunasababishwa na maambukizi.

ENDOSKOPI

Endoskopi ni jina la jumla la aina ya vipimo ambayo inaruhusu daktari maalum (mtaalamu wa endoskopi) kuangalia moja kwa moja ndani ya mfumo wa utumbo, kwa kutumia endoskopu. Ikiwa mgonjwa atakisiwa kuwa na IBD, anashauriwa kumwona daktari wa matibabu au upasuaji wa matumbo ili kufanyiwa uchunguzi wa endoskopi.

Katika uchunguzi wa endoskopi daktari au mtaalamu wa endoskopi hutumia endoskopu – bomba ndefu nyembamba, ambalo kwa kawaida hunyumbulika, lenye kamera kwenye ncha yake – kuchunguza mfumo wako wa umeng’enyaji chakula. Kuna aina kadhaa za endoskopi ambazo zinaweza kuwa na majina tofauti kulingana na sehemu ya utumbo inayochunguzwa.

Endoskopi ya sehemu ya juu ya mfumo wa umeng’enyaji chakula au uchunguzi wa matumbo hutumiwa kuchunguza sehemu ya juu ya mfumo wako wa kumeng’enya, kama vile umio na tumbo. Kifaa huingizwa kupitia mdomoni.

Uchunguzi wa koloni au sigmoidoskopi hutumiwa kuangalia koloni. Sigmoidoskopu (endoskopu fupi) au kolonoskopu (endoskopu ndefu na inayonyumbulika zaidi) inaingizwa kupitia njia ya haja kubwa (njia ya nyuma) ili kuchunguza puru na koloni.

Shughuli ya endoskopi haipaswi kuwa chungu lakini inaweza kuwa na wasiwasi, hivyo unaweza kupewa dawa za kutuliza ili kukusaidia kupumzika. Bayopsi (sampuli ndogo za tishu) mara nyingi huchukuliwa wakati wa endoskopi. Hizi zinaweza kuchunguzwa chini ya darubini ili kusaidia kuthibitisha utambuzi wa IBD.

Endoskopi ya kidonge ni aina maalum ya endoskopi ambapo unameza kamera ndogo (karibu kutoshana na zabibu ndogo) ambayo hupitia mfumo wa kusaga chakula, ikichukua picha za ndani ya utumbo. Picha hizi hupitishwa kwa kinasa data kinachovaliwa kiunoni.

Kidonge hiki hutoka nje ya mwili kwa njia ya kawaida katika harakati ya kwenda haja kubwa. Sio vituo vyote vinavyotoa endoskopi ya vidonge, na pia haiwezi kutumika na kila mtu kila mtu.

EKSIREI YA TUMBO NA UCHUNGUZI WA TOMOGRAFIA YA KOMPYUTA

Kuna aina nyingi tofauti za eksirei zinazotumiwa katika IBD. Eksirei ya fumbatio tupu inaweza kutumika wakati wa dharura au katika kutambua watu walio na IBD.

Uchunguzi wa tomografia ya kompyuta hutumia msururu mzima wa picha za eksirei ili kupiga picha ya kina ya mwili. Kitambazaji kina umbo la donati, na mionzi ya eksiei huchukuliwa kwa pembe tofauti, picha zinazotolewa huwekwa pamoja ili kutoa sehemu mtambuka (pande mbili) za mwili.

Mfumo wa umeng’enyaji chakula hauonyeshi vizuri katika picha za eksirei, kwa hivyo unaweza kupewa bariamu ili kusaidia kupiga picha iliyo wazi zaidi. Hii ni dutu nyeupe isiyo na madhara ambayo haifyonzwi mwilini, lakini badala yake huunda mipako ya muda ndani ya utumbo. Miunzi ya eksirei haiwezi kupita kwenye bariamu, kwa hivyo hii inatoa muhtasari wazi wa utumbo katika picha za eksirei. Bariamu inaweza kutolewa kama kinywaji ili kusaidia kuonyesha matatizo katika utendakazi wa tumbo au utumbo mdogo, au katika enema ili kuonyesha kuvimba kwenye koloni.

KIPIMO CHA PICHA YA TIBAMAWIMBI CHA TUMBONI

Vichanganuzi vya kipimo cha picha ya tibamawimbi hufanya kazi kwa kutumia mawimbi ya sauti ya masafa ya juu sana ili kupiga picha. Kihisi kinachoshikiliwa mkononi husogezwa juu wa ngozi, ambacho hutuma ishara za mawimbi ya sauti ambazo huchukua viungo vya ndani kama mwangwi. Kitambazaji kisha huchukua mwangwi na kuzibadilisha kuwa picha.

Vipimo vya kipimo cha picha ya tibamawimbi vinaweza kutumika kutafuta vijiwe kwenye nyongo na figo. Pia hutumika katika kugundua mikusanyo ya viowevu na sehemu za ukuta wa matumbo zenye unene na zilizovimba. Kipimo cha picha ya tibamawimbi kinaweza pia kuonyesha jipu na fistula (njia zisizo za kawaida zinazounganisha sehemu tofauti za matumbo).

UCHUNGUZI WA MRI

Uchunguzi wa MRI hutumiwa kupiga picha za sehemu tofauti za mwili. Njia hii hutumika zaidi kuchunguza IBD, hasa kwa watoto, ili kuepuka matumizi ya eksirei. Badala yake, hutumia nyuga zenye nguvu za sumaku na mawimbi ya redio kupiga picha za ndani ya mwili.

Uchunguzi wa MRI hutumiwa kupiga picha za sehemu tofauti za mwili. Njia hii hutumika zaidi kuchunguza IBD, hasa kwa watoto, ili kepuka kutumia eksirei. Badala yake, hutumia nguvu za sumaku na mawimbi ya redio kupiga picha za ndani ya mwili.

Kichanganuzi cha MRI kinaonekana kama bomba au handaki ndefu, ambapo utaombwa ulale kwenye meza inayoweza kusogezwa ambayo inateleza polepole ndani ya handaki hili. Uchunguzi wa MRI ni njia nzuri ya kuchunguza tishu laini kama vile misuli na utumbo, pamoja na viungo kama vile ini. Hii ni kwa sababu ni nzuri sana katika kugundua fistula (njia zisizo za kawaida zinazounganisha sehemu tofauti za matumbo), na jipu, na kutofautisha kati ya uvimbe na kovu.