Vidonda vya Koloni ni nini?

Vidonda vya koloni ni aina ya uvimbe wa matumbo ambayo huathiri tu koloni.

Inasababisha kuvimba kwa tabaka za juu za koloni kwa kiwango tofauti na kusababisha “kolitisi”, yaani kuvimba kwa koloni. Kuvimba kwa kidonda kunaweza tu kuathiri puru (proktitisi) au koloni nzima (jumla au “pankolitisi”. Kuendesha, damu na kamasi kwenye kinyesi, na maumivu ya tumbo ni baadhi ya dalili za kawaida za vidonda vya koloni.