Ugonjwa wa Crohn ni nini?

Ugonjwa wa Crohn ni aina ya uvimbe wa matumbo au IBD.

Ugonjwa wa Crohn unaweza kuathiri sehemu yoyote ya njia ya utumbo kuanzia mdomoni hadi kwenye njia ya haja kubwa lakini kwa kawaida huhusisha sehemu ya mwisho ya utumbo mwembamba, au ileamu ya mwisho, na koloni. Mara nyingine ugonjwa wa Crohn huhusisha tabaka za ndani zaidi za utumbo ambao huipa uwezo wa kipekee wa kutengeneza fistula, aina ya ugonjwa ambao huchimba kupitia utando wa utumbo. Fistula inaweza kutokea mahali popote kwenye utumbo ikiwa mtu ako na ugonjwa wa Crohn lakini mara nyingi hutokea karibu na njia ya haja kubwa (fistula ya pembeni mwa mkundu). Maumivu ya tumbo, kupoteza uzito, uchovu na mabadiliko ya tabia ya matumbo ni dalili za kawaida za ugonjwa wa Crohn.